Ugonjwa wakisukari [diabetes]


 Ugonjwa wakisukari [diabetes]

Ugonjwa wa kisukari umekuwa tatizo sana katika jamii zetu za sasa kutokan na mfumo wa maisha tuliojiwekea sisi wenyewe.
Kisukari ni ugonjwa chronic ambao huambatana na ongezeko la sukari [glucose] mwilini.
Sukari huingia kwenye mwili na kuingia kwenye mihipa ya damu kupitia vyakula tunavyokula,na kuna ogani ndani ya mwili inayopatikan maeneo ya tumbo ambayo hufanya kazi ya kuratibu kiwango ch asukari ndani ya mwili ambayo ogani iyo huitwa kongosho [pancrease] amabyo hutoa chemikali inayoitwa insulin ili kusawazisha kiwango cha sukari kinachohitajika kwenye mwili wa binadamu. Pia insulin hupeleka kiwango cha sukari katika muscle,maini na sehemu nyingine.
 Sasa kongosho/insulini zinaposhindwa/kuzidiwa kuratibu kiwango cha mwilini hapo mtu anaweza kupata kisukari.


Aina za kisukari
1.type 1 diabets/onset diebet [kisukari aina ya kwanza]
Hii hutokea kwasababu mwili wa mototo unakuwa hauna uwezo/huzalisha insulin kwa kiwango kidogo.
ü  Hii huweza kujitokeza wakati wa utoto.
ü  Wakti mwengine huwa haina dalili
ü  Na watu wa aina hii wanaitaji kuwa wanaongezewa insulin ili waweze kuishi
ü   
2.type 2 diebetes
Hii hutokea kutokana na mfumo mbaya wa ulaji chakula ,unene wa kupita kiasi na kutokufanya mazoezi. Hivyo kiwango cha sukari mwilini insulin inashindwa kukiratibu
Ø  Hii ni aina ya kisukari ambayo ipo sana kwa watu
Ø  Inatokea katika umri wa watu wakubwa lakini huathiri san watoto

3.getastion diabetes [kisukari kipindi cha ujauzito]
Hii huwapata akina mama wajawazito kwasababu
§  Kiwango cha sukari kwa mama mjamzito huongezeka

4.pre diabetes  [kisukari ]
Imefikia kiwango cha watu milioni 79 duniani ambao wanapimwa na kukutwa na kiukari
Mtu anakuwa na kiwango kikubwa cha sukari ndani ya mwili ambacho huwezi linganisha na aina za kisukari kingine tulichokitaja hapo juu.
Aina hii ya kisukari huweza kuathiri sehemu mbali mbali za mwili wa binadamu kama moyo,na mfumo wa damu kwa ujumala.


Dalili za ugonjwa wa kisukari
§  Kiwango kikubwa cha sukari mwilini
§  Kuona hafifu [kuona ukungu ukungu]
§  Mwili kuihiwa nguvu
§  Kiu mara kwa mara
§  Maumivu wakati wa kukojoa
§  Kukojoa mara kwa mara
§  Vidonda ambavyo haviponi
§  Kichefuchefu
§  Kupungua uzito
§  Kutapika
§  Njaa mara kwa mara

Ikumbukwe kwa baadhi ya kisukari hizi dalili unaweza usizione mfano mtu mwenye kisukari aina ya kwanza.

Kisukari si ugonjwa wa kuambukiza
§  Kwa kisukari aina ya kwanza,kisukari wakti wa mimba,na aina ya mwisho hii inatokan na kurithi
§  Kisukari pia huweza kutokea kwa ulaji mbaya wa chakula,kutofanya mazoezi
§  Wakati mwingine kisukari kinaweza kusababishwa na
                                                    Unene kupita kiasi
                                                      Presha ya kupanda
                                                     Kiwango kikubwa cha cholesterol
                                                      Historia ya famila
                                                     
Jinsi ya kuepuka /kupunguza kisukari

§  .kubadili mfumo wa maisha mfano ulaji na mazoezi,
§  Kutumia dawa kama ulivyoelekezwa na daktari
§  Kuwa mwangalifu na mwili wako
§  Angalia preha yako mara kwa mara ili uweze kuimaintain
§  Epuka uvutaji wa sigara

Athari za ugonjwa wa kisukari


Ugonjwa wa kisukari  huweza kuathiri
Moyo,figo,macho,mfumo wa mishipa ,ngozi,mwili wote[kupararaizi,matatizo ya moyo,stroko.vidonda visivyopona
Mwisho wa siku hupelekea kifo.



Post a Comment

0 Comments