UFAHAMU UGONJWA WA SIKO SELI [SICKLE CELL DISEASE].
Sickle cell ni ugonjwa wa kurithi ambao motto/mtu anaweza
kupata kutokana na hitoria ya baba au mama au familia ya baba na mama kuwa na
ugonjwa huo [genetic disease].ugonjwa huu hutokea kwenye mwili wa binadamu
kwenye chembechembe nyekundu za damu [red blood cell] ambazo huweza kubadilisha
umbo ,ukubwa,mpangilio na hivyo kupoteza uhalisia wake na kusababisha ugonjwa
huu wa sickle cell.
Umeitwa sickle
cell kwasabu kwa kawaida chembe chembe nyekundu za damu zina umbo lake na sifa
zake [biconcave disc] yani mfano wa disk iliyobonyea sasa inapotokea mabadiliko
hayo hubadili umbo na kuwa sickle [mfano wa panga la kukatia majani ya ngombe]
ndo maana ukaitwa sickle cell disease.
Aina
za ugonjwa wa sickle cell
Sickle
cell anemia –hii inatokea pale ambapo mtu hemoglobin zake zote zinazofanana
zinakuwa zimeathirika [HbS,HbS].na hii ndio inakuwa na athari kubwa kwa mwenye
nayo maana mgonjwa huyu atakuwa na upungufu wa damu mara kwa mara
Sickle cell
trait-hii hutokea pale ambapo mtu hemoglobin zake zote ambazo hazifanani ambayo
hemoglobin moja inakuwa nzima nay a pili inakuwa imeathirika na sickle cell
[HbS,HbA]
Dalili za
ugonjwa wa sickle cell
Kwa kawaida ikiwa motto atazaliwa na ugonjwa huu
katika kipindi cha kwanza cha miezi sita huwa haoneshi dalili za ugonjwa huu.
Miongon mwa dalili za ugonjwa huu wa sickle cell ni
kama zifuatazo.na dalili hizi tunaweza kuziweka katika makundi makundi.
1.dalili zinazotokea katika miguu na mikono [hand-foot syndrome]
Dalili
hizi huambatana na dalili zifuata
Maumivu ya mikono na miguu
Kuvimba kwa mikono na miguu
2. maumivu ya mara kwa mara [pain epsode]
Hii kwa watoto wadogo huwathiri sana na kuwa na
maumivu mara kwa mara
Kwa watu wakubwa wenye sickle cell maumivu huttokea
kichwani,kifuani,maeneno ya tomb,na nyuma ya mgongo
Na maumivu huwa yanatokea mara kwa mara katika
sehemu moja iyoyo
Homa za mara kwa mara,kupungukiwa na hewa safi
[oxygen] yaani hypoxia
3.maumivu
katika mishipa ya damu
4.kuvimba kwa
bandama
5.kupungukiwa kwa damu mara kwa mara [japo si kila
anaepungukiwa na damu mar a kwa mara ana ugonjwa huu]
6.macho kuwa ya manjano pia mweny manjano ana
ugonjwa huu,ngozi kupauka pallor
7.maumivu na kusimama kwa uume ovyo ovyo kitaalamu
wanaita priapism
8.vidonda kwenye miguu
9.kuchomoza kwa meno ya mbele,paji la uso [frontal bossing] protrusion of upper teeth .pia si kila mwenye
meno yaliyotokeza anaugonjwa huu
Jinsi ya kumeneji ugonjwa wa sickle cell
- · Uchunguzi wa awali na kufanya ufuatiliaji mara kwa mara
- · Epuka sababu ambazo zinaweza kufanya cell kuwa sickle hii ina maana kwamba kwa mgonjwa wa siko seli anahitaji hewa safi ya kutosha inayozunguka ndani ya damu ili asipate matatizo hivyo basi kuna baadhi ya vitu vikifanyika sana kwa mgonjwa huyu anaweza kuzidiwa mfano wa vitu hivyo ni kufanya mazoezi sana/kwa muda mrefu,stress nyingi,kunnywa maji kidogo,baridi,maradhi mengine,uvutaji wa sigara,
- · Jizuie na magonjwa mengine
- · Folic acid supplementation
- · Jifunze elimu ya afya na ushauri
- · Kuongezea damu kwa yule alieishiwa
- · Prescribe medication .dawa sahihi kutoka kwa daktari (see also other disease)
NB: SICKLE CELL NI UGONJWA WA KURITHI NA DALILI ZAKE
ZINAWEZA KUONEKANA IKIWA ZITAFANYIWA UCHUNGUZI MAPEMA NA HIVYO KWA KUFUATA KUISSHI KIAFYA SAHIHI KWA KUPATA ELIMU JU YA
UGONJWA HUU,NA UZALENDO WA KUFUATILIA CLINIC MARA KWA MARA UNAWEZA KUISHI
SALAMA KWA KIPINDI KIREFU.
0 Comments