VIRUSI
VYA HOMA YA INI [HEPATITIS]
Virusi
vya homa ya Ini
Ugonjwa wa
homa ya ini ni hatari kuliko ukimwi,uwezekano wa mtu kupata maambukizi ya
virusi vya homa ya ini ikiwa atajamiana na mtu mwenye virusi hivyo ni mara 10
zaidi ikilinganishwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Takwimu zinaonesha
zilizotolewa mwanzoni mwa mwaka huu nchini ni kuwa watu nane kati ya 100 nchini
wana maambukizi ya virusi vya homa ya ini hususani hepatitis B.
Saratani
ya ini inasababishwa na nini?.
Ugonjwa
huu unaweza kusababishwa na vitu
vifuatavyo
1.saratani
ya ini inayotokana na kuzidi sumu kwenye ini [toxic hepatitis]
Hii inaweza
sababishwa na madawa ,utumiaji pombe kupita kiasi,sumu za viwandani,sumu za
miti.
2.saratani
inayotokana na unywaji wa pombe kupita kiasi [alcholic hepatitis]
Hii inaweza
kuwa sugu au isiwe sugu na inaweza kutibika ikiwa mtu ataacha matumizi yapombe
yaiofaa.na hii ndio inaweza kusababisha kulika/vidonda kwenye ini.
3.saratani
inayosababishwa na virusi [viral hepatitis]
Hapa tuna
tizama virusi wanaosababisha ugonjwa huu ambao ni
Virusi vya
hooma ya ini aina A [HEPATITIS A],virusi vya homa ya ini aina B [HEPATITIS B],Virusi
vya homa ya aini aina C [HEPATITIS C],virusi vya homa ya ini aina D [HEPATITIS D] NA HEPATITIS E
JINSI UNAVYOAMBUKIZWA:
Katika
maeneo hatari zaidi duniani, Virusi vya Hepatitis B (HBV) kwa kawaida
husambazwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa au kutoka kwa
mtu mmoja hadi mwingine hususan nyakati za utotoni.
Kama
ilivyo kwa Ukimwi, Virusi vya Homa ya Ini pia huambukizwa kwa njia ya
kujamiiana, mate, jasho na mwingiliano wowote ule wa damu.
Njia kuu
za maambukizi :
-Kujamiana
bila kinga
-Kunyonyana
ndimi 'denda'
-Mama
mwenye ugonjwa kumwambukiza mtoto wakati wa
kujifungua
-Kuchangia
damu isiyo salama
-Kuchangia
vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kuchangia
miswaki
-kuchangia
taulo na mwenye ugonjwa huo
-kubadilishana
nguo au kukumbatiana wakati mkiwa mnavuja jasho.
Mtu
mwenye Homa ya Ini ana wastani mdogo wa kuishi kuliko mwenye Ukimwi. Kwa maana
hiyo, mwenye maambukizi ya Virusi vya Homa ya Ini hufariki dunia haraka kuliko
mwenye VVU.
Dalili
za saratani ya ini.
•Liver Cirrhosis (vidonda kwenye ini).
·
Watu
wengi hawaonyeshi dalili yoyote. Kwa maana hiyo mtu anaweza kuishi na HBV na
kusababisha maambukizi kwa wengine bila kugundulika.
·
Hata
hivyo, watu wengine husumbuliwa na homa kali na dalili ambazo hudumu kwa wiki
kadhaa. Dalili hizo ni:
-Uchovu
-Kichefuchefu
-Mwili
kuwa dhaifu
-Homa
kali
-Kupoteza
hamu ya kula
-Kupungua
uzito
-Maumivu
makali ya tumbo upande wa ini
-Macho
na ngozi kuwa vya njano
-Mkojo
mweusi
Kwa
wagonjwa wengine, Virusi vya Hepatitis B hukua hadi kusababisha ini kuharibika
kabisa (cirrhosis of the liver) au saratani ya ini (liver cancer).
matibabu
ya virusi vya homa ya ini
Gharama za kutibu ugonjwa huu ni kubwa na ni vyema jamii ikajikinga na ugonjwa huu hatarishi.
Alisema ummy
mwalimu “kinga ni bora kuliko tiba ,tiba kwa wagonjwa waliopata kirusi aina A
NA E ,mara nyingi hutolewa kutokana na dalili zinazoambatana na ugonjwa huu”
kwa wagonjwa waliogundulika kuwa na hepatitis B na C matibabu hutegemea na
hatua aliofikia.
Kinga
ya ugonjwa huu
1.Chanjo/kinga
.Kinga hii hutolewa kwa mtu ambae hana maambukizi ya virusi hawa.
Na chanjo
iliopo kwa Tanzania ni ya hepatitis B.Chanjo ya hepatitis A inapatikana baadhi ya
nchi
Na hakuna
chanjo kwa hepatitis C,D na E.
2.Kuepuka
matumizi ya madawa ya kulevya
3.kuepuka
uasherati
4.kujiepusha
matumizi mabaya pombe
-Kuacha
kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kutochangia
miswaki
KUNDI
LIPI NI HATARI ZAIDI?
Asilimia
80-90 ya watoto wachanga ambao huambukizwa katika kipindi cha mwaka wa kwanza
tangu kuzaliwa, Homa ya Ini hukua mpaka kufikia kuwa sugu na hatimaye kifo.
Asilimia
30-50 ambao huambukizwa kabla ya kufikisha umri wa miaka sita, Hepatitis B
hukua mpaka kuwa sugu na baadaye ni kifo.
Asilimia
90 ya watu wazima wanaopata HBV, virusi hivyo hutoweka ndani ya miezi sita.
Yaani uimara wa ini husababisha virusi hivyo kupotea.
Asilimia
tano kushuka chini ya watu wazima wanaopata maambukizi ya HBV, virusi hivyo vya
Hepatitis B kugeuka sugu na hatimaye kifo.
Asilimia
15-25 ya watu wazima ambao walipata maambukizi utotoni na hatimaye Hepatitis B
kuwa sugu, hufariki dunia kutokana na matokeo ya ini kuharibika kabisa au kwa
saratani ya ini.
TANZANIA
IPO KUNDI HATARISHI
Kwa
mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Kusini ya Jangwa la
Sahara ndiyo eneo hatari zaidi. Tanzania ni moja ya nchi zilizopo katika eneo
hilo. Kiwango cha hatari Kusini ya Jangwa la Sahara kinalingana na kile cha
Mashariki ya Bara la Asia.
Ripoti
hiyo inaonesha kuwa watu wengi walipata maambukizi nyakati za utotoni na kwamba
kati ya asilimia tano mpaka 10 ni waathirika sugu.