TATIZO LA KUKOSA USINGIZI [INSOMNIA]


TATIZO LA KUKOSA USINGIZI [INSOMNIA]


Tatizo la kukosa usingizi huu ni ugonjwa wa mtu kukosa usingizi  kwa kusumbuka kulala au kukaa muda mrefu bila usingizi.au kuhindwa kubalani ratiba yake ya ulala

Watu wenye tatizo la kukosa usingizi  wana sifa zifuatazo
1.ugumu/shida ya kupata usingizi nyakati za usiku
2.kuamka wakati wa usiku na kupata shida ya kurudi tena kwenda kulala
3.kuamka mapema san nyakat za asubuhi
4.kujisikia uchovu mara kwa mara unapotoka uingizini


Sababu zinazopelekea  tatizo la kukosa usingizi.
1 mfadhaiko [stress] na wasiwasi
Watu huweza kupata tatizo la kukosa usingizi kwasababu ya mifadhaiko walio nayo
Mfano matatizo kazini au matatizo ya kifedha.
2.ratiba mbovu ya kulala na sehemu ya kulala
Unaweza hangaika kupata usingizi ikiwa endapo utakwenda kulala mida mibovu pia mazingira mabya nayo huweza changia mtu akose usingizi.mfano mtu kulala pahala ambapo hayuko huru napo au chumba kina mwanga mkubwa,makelele ,joto au baridi.
3.mfumo wa maisha
Kunywa pombe usiku,au mirungi na kwenda kitandani inaweza athiri usingizi wako.pia kubadilisha muda ambao umezoea kulala pia inaweza kuathiri uingizi wako
4.matatizo ya akili
Pia wengi wenye matatizo ya ubongo hii pia huweza kuwasababishia wao kukosa usingizi vizuri.
5.matatizo ya mwili kiujumla [physical health condition]
Mfano wa maradhi haya yanaweza mkosesha mtu usingizi matatizo ya moyo,,matatizo ya upumuaji,matatizo ya neva na mengine mengi.

6.madawa  [medication]
Yapo madawa ambayo maeleezo yake anapotumia mtu huweza mkosesha mtu usingizi.mfano dawa zilizo na antidepressant,madawa ya presha ya kupanda.


Hasara za kukosa usingizi
Kulala ni muhimu san kwa afya  yako kama ilivyo kwnye kula chakula chenye afya na kufanya mazoezi.tatizo la kukosa usingiz ina sababisha matatizo kwnye akili na kwenye mwili.
1.inaweza kushusha ufanisi katika kazi au shuleni
2.inaweza kusababisha disorder mablailmbali katika ubongo mfano mood disorder
3.kupata uzito kupita kiasi



Natibabu ya kukosa usingizi
1.kupumzika na kufanya mazoezi
2.kupewa dawa [sleeping pills]
3.kupunguza mfadhaiko na wasiwasi


Post a Comment

0 Comments