KANSA YA TEZI DUME [PROSTATE CANCER]

Billyblogtz
0

KANSA YA TEZI DUME [PROSTATE CANCER]


Kansa ya tezi dume ni moja ya aina ya kansa ambayo hutokea sana kwa upande wa wanaume na huweza kusasababishia kifo  ikiwa haitafanyiwa ufumbuzi wa harakaa
Uvimbe huanza kutokea katika katika tezi ya mwanaume itwayo prostate gland.
Kansa zingine za tezi dume hukua kwa taratibu sana na mtu anaweza asijisikie kama anaumwa ugonjw huu kwa kiasi cha miaka mingi.

Kundi lipi liko hatarini Zaidi kupata ugonjwa huu au kansa ya  tezi dume
 Umri>kadri ya umri unavyozidi kuongezeka kwa upand e wa mwanaume ndivyo anvyozidi kuwa na uwezekano wa kupata ugonjwa huu

Hitoria ya familia>ikiwa kama wanaume katika familia yenu walikuwa wanaumwa au wshawahi kuumwa ugonjwa huu kuna uwezekano pia kuathiri mtu anaetoka katika familia hio.

Obesity [unene kupita kiasi]>wanaume walio wanene kupita kiasi pindi wakikutwa na ugonjwa huu inaweza kuwa kazi kuwatibu.

Lishe>upungufu mwingi wa vitamin D nao pia inaongeza asilimia za mtu kupata ugonjwa huu

Matatizo ya homoni>kupanda ana kwa kiwango cha homoni ya kiume [testeosterone] nayo ina ongeza asilimia za mtu kuugua ugonjwa huu.


Uchunguzi wa awali wa kansa ya tezi dume [prostate cancer]

1.kuutumia PSA [Prostate specific antigen test] hii hupimwa maabara

2. kuchunguza sehemu ya nyuma [digital rectal examination]

3.uchunguzi wa awali katika chumba cha daktari [discuss screening with your doctor]


Dalili za kansa ya tezi dume
o   Kukojoa mara kwa mara,au kidogo,kukatika katika kwa mkojo wakati unakojoa
o   Maumivu au kuhisi kama unaungua kipindi unapokojoa,damu kwenye mkojo
o   Kubanwa sana na mkojo mara kwa mara wakati wa usiku
o   Kama kansa imeshasambaa au kuwa kubwa mtu anaweza onesha dalili za kuuma kwa mgongo,kupungua uzito,na kukosa nguvu

Ikumbukwe wakati mwingine wagonjwa wa tezi dume hawaoneshi dalili hizi,na dalili hizi mtu anaweza kuziona lakini ikawa ni dalili za magonjwa mengine na si za tezi dume.ili kuhakikisha ukiona dalili hizi nenda hospitali iliyo karibu nawe upate ushauri wa daktari na vipimo.


Hatua za kansa ya tezi dume



Kuna hatua kama nne za kansa ya tezi dume .na hatua hiz huangaliwa na daktari kwa kutizama ni namna gani uvimbe upoje na umeenea kwa kiasi gani.

Hatua ya kwanza [stage I]
Hapa tunasema kansa meathiri tu kwenye tezi husika yani prostate

Hatua ya pili [stage II
Kansa haijaenda mbali kwenye tezi [prostate] lakini imeanza kushambulia sehemu nyingi za tezi hiyo

Hatua ya tatu [III]
Kansa inaanza kusamba kutok akwenye tezi [protate] na kuanza kushambulia sehemu inayo zalisha mbegu za kiume [seminal vesicle]

Hatua ya nne [stage IV]
Kansa inaanza kuenea sehemu nyingine za mfumo wa uzazi,upumuaji na mkojo wa mwanaume kama  kibofu,kwenye ngozi ya korodani,sehemu kunakopitishaa kinyesi [rectum],
Mapafu na sehemu nyinginezo.


Matibabu ya tezi dume
Matibabu yanategeme na hatua ya mgonjwa yuko kwenye hatua ipi ya ugonjwa
§  Njia Zaidi ya moja ya matibabu inaweza kutumika
§  oporesheni [kuondoa prostate gland]

  
§  Kutibu kwa kutumia mionzi


§  Kutibu kwa kutumia homoni [kwa kupunguza homoni za kiume kukua kwa taratibu ili kupunguza 
ukuaji wa kansa nah ii inaweza kusababisha madhara mengi]

§  Chemotherapy

§  Na matumizi ya dawa kwa maelekezo ya daktari
   

Asnte kwa kuendelea kufuatilia matangazo yetu

Kuwa wakwanza kupata habari na taarifa mbalimbali kwa kubonyeza 

Tags

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(1)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!