Nurse (Muuguzi) - Readvertisement
Sense
International (EA) Tanzania
Dar es
Salaam
Full
Time
Healthcare
TSh Confidential
Job
Summary
Screening
nurse
Minimum
Qualification: Diploma
Experience
Level: Mid level
Experience
Length: 2 years
Job
Description
Sense
International ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya shughuli za kuhudumia
jamii ya watu wenye ulemavu wa uziwikutoona (Deafblindness) ili waweze
kujifunza,kuishi na kufanikiwa. Aidha, shughuli za shirika zipo nchini
Bangladesh, India, Nepal, Tanzania, Peru, Romania na Uganda. Nchini Tanzania,
Sense International inashirikiana na serikali na asasi mbalimbali katika
kuwatambua watu wenye uziwikutoona kisha kuwawezesha kielimu, kiafya na namna
ya kujikimu kimaisha ili waweze kushiriki na kuchangia maendeleo ya jamii.
Ili
kuhakikisha ya kwamba mabadiliko ya utoaji huduma yanakuwa endelevu shirika
linawekeza katika kufanya ushawishi wa mabadiliko ya sera ili ziakisi utoaji wa
huduma kulingana na mahitaji ya watu wenye ulemavu, kujenga mazingira wezeshi
ya utoaji wa huduma za elimu na afya kwa watu wenye uziwikutoona pamoja na
kuwaendeleza na kuwatumia wataalamu wazawa.
Hivi
sasa Sense International Tanzania kwa kushirikiana na Manispaa ya Temeke
inahitaji wauguzi kwa ajili ya kufanya kazi katika mradi wa kufanya Utambuzi na
utoaji wa Afua za Mapema (Early Intervention) kwa watoto wenye uziwikutoona na
wenye ulemavu mwingine mchanganyiko kuanzia miaka 0-5. Mradi huu ni wa ufadhili
wa Jessey Overseas Aid (JOA) kutoka nchini Uingereza.
WAUGUZI
–NAFASI 4
Wilaya:
Temeke
Mkoa:
Dar es Salaam
Muda wa
ajira: Miaka 2 au zaidi kutegemeana na uwepo wa ufadhili.
Mshahara:
Mshahara mzuri sambamba na marupurupu.
Majukumu
ya kazi:
· Kufanya upimaji wa milango ya fahamu
(uoni na usikivu) kwa kutumia vifaa maalumu katika vituo vya kutolea huduma.
· Kutumia dodoso maalumu kubaini
viashiria hatarishi kwa watoto ambao bado hawajapimwa na kutumia vifaa maalumu
pale inapohitajika.
· Kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa
mtaalamu wa Tiba Liwaza (Occupational Therapist) ili kuweza kuandaa mpango
madhubuti wa utoaji Afua za Mapema kwa watoto wanaopatikana na uziwikutoona au
ulemavu mwingine Mchanganyiko unaopelekea changamoto za mawasiliano na
kujimudu.
· Kutoa ushauri kuhusu changamoto
mbalimbali katika vifaa vinavyotumika kuwasaidia watoto wenye uziwikutoona.
· Kushirikiana na mtaalamu wa tiba
liwazo, wazazi na watoto katika kusadia maendeleo ya watoto wenye uziwikutoona.
· Kutunza kwa makini vifaa vilivyopo
katika kituo cha kutolea huduma.
· Kuagiza kwa wakati vifaa muhimu vya
kutumiwa katika kituo cha kutolea huduma.
· Kutumia mifumo iliyopo ya kusimamia na
kutoa taarifa kuhusu utoaji huduma za Upimaji na Usaidizi wa awali.
· Kushiriki katika kuelimisha jamii
kuhusu huduma ya upimaji na usaidizi wa awali katika kituo cha kutolea huduma
katika jamii na mahali pengine utakapohitajika.
Tunatafuta
muuguzi mwenye uzoefu katika kazi ya uguuzi, kuhudumia watu kwa weledi,
kuwasiliana vizuri na kutoa taarifa ya maendeleo kwa wakati na umakini.
Vigezo
vya mwombaji:
Awe na
“Diploma” ya uuguzi kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
Awe
mwanachama wa Baraza la cha Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nursing and
Midwifery Council).
Awe na
uzoefu wa kazi usiopungua miaka 2.
Awe na
zoefu wa kusaidia watoto wenye ulemavu
hususani watoto wenye Uziwi-kutoona (Deafblindness).
Kufahamu
zaidi kuhusu kazi zetu, tembelea:
https://www.senseinternational.org.uk/our-work/tanzania
Kama una
vigezo stahiki na ungependa kuomba kazi hii, tuma barua yako ya maombi na
wasifu wako kwa Mkurugezi, Sense International Tanzania, P O BOX 72653, Dar es
Salaam kupitia infotz@senseint-ea.org. Unapotuma barua pepe, weka kichwa
(SUBJECT) MUUGUZI – TANZANIA. Tafadhali elezea kwenye barua yako ya maombi;
sababu za kupendezwa na nafasi hii, ni kwa jinsi gani ujuzi na uzoefu wako
unashabihiana na kazi hii, pia elezea mshahara unaopokea sasa pamoja na namba
yako ya simu inayopatikana. Mwisho wa kutuma maombi ni saa 11 kamili jioni,
tarehe 12 Novemba, 2018. Ni wale tu waliofuzu ndio watapokea majibu.
Sense
International inaajiri bila kuzingatia jinsia, dini, rangi, kabila, uraia,hali
ya ulemavu au namna yoyote ya ubaguzi.